Mto Imo

Mto Imo

Mto Imo ni mto nchini Nigeria.

Chanzo chake kinapatikana Okigwe kwenye jimbo la Imo. Unaishia kwenye bahari ya Atlantiki. Mto huu unalisha eneo la kinamasi lenye ukubwa wa heka 26,000 na ujazo wa kilomita za ujazo 4 za maji ya mvua kwa mwaka.

Jamii zinazokaa pembezoni mwa mto zinaamini kuna mungu wa kike anayeitwa Imo Mmiri ndiye anayemiliki mto huo.[1]

  1. Uzor, Peter Chiehiụra (2004). The traditional African concept of God and the Christian concept of God. Peter Lang. p. 310. ISBN 3-631-52145-6.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy